KUHUSU LEONARD
Leonard Jacobson ni mwalimu wa mambo ya kiroho, yeye hujaribu kumshiriki mungu kwa kujitoa na kutafakari sana habari za mungu na pia ni mponyaji hodari. Leonard amejipa sharti kuwasaidia wengine kufanikiwa kuonja raha ya kuishi katika SASA. Ana uwezo wa kimaajabu wa kujiweka katika hali ya kila mtu na kwa upole kuwaongoza katika ukamilifu, uaminifu na katika hali ya kuzinduka.
Amekuwa akiendesha maisha na kongamano kwa miaka ishirini na tano iliopita kutoa shauri na maongozi kwa wale walio katika njia ya mwamko na kuerevuka kiroho. Mafundisho na uwepo wake ni kumbusho la nguvu kwamba asili ya maisha na ukweli iko katika kila mmoja wetu.
Katika mwaka wa 1981, alipata kuona safu ya kwanza ya mafumbo ya moyo na mwamko ulio badili kwa ndani ufahamivu wa maisha, ukweli na haki. Kila moja ya mambo ya maisha ya kuerevusha ilifichua kwa undani na kwa undani zaidi usawa wa kufahamu moyoni, kujaza mafunzo na maandiko yake na busara ya maana, uwazi, upendo na huruma.
Anaishi Santa Cruz, California na hutoa mafunzo ya jioni, warsha za mwisho wa juma, na kongamano huko Marekani, Uropa, na Australia.
Yeye ndiye mwanzilishi wa 'The Conscious Living Foundation,' shirika lililo sajiliwa na lisilo la kutoa faida katika mwaka wa 2005, alituzwa zawadi la amani na 'Religious science international' ingawaje yeye hajihusishi na dini au kanisa yoyote.
Mafunzo yake hujumuisha ndani yake dini zote na mazoea ya kiroho. Ni kwa wale wote wanaotafuta mzinduko wa kweli na kwa wale wote ambao bado hawajui kwamba wanatafuta mzinduko wa kweli.
Yeye ndiye mwandishi wa vitabu vinne
Word from silence, Embracing the present, Bridging Heaven & Earth na
Journey into Now, ambalo ndilo toleo la mwisho zaidi.
TOLEO LA MWISHO
Kitabu cha nne na cha mwisho cha Leonard kwa sasa kinapatikana katika website yetu. Hakitapatikana katika maduka ya vitabu hadi Machi, 2007.
Journey into Now (Safari kuingia sasa):
Maongozi ya wazi katika njia ya mwamko wa kiroho
Kila wakati sisi hukumbana na kitabu kinachoweza kubadili maisha yetu na kutuinua katika lengo jipya la ufahamu wa moyoni. Journey into Now (Safari kuingia Sasa) ni kitabu cha namna hii. Kwa utaratibu ulio kamilika, mwandishi anamwongoza msomaji katika njia ya mwamko ambao huongoza katika kuwa huru kutokana na uchungu na vizuizi vya zamani kuingia dunia ya sasa isio na mpaka na yenye furaha. Hiki kitabu kina dhihirisha kwa njia ilio rahisi jinsi ya kutuliza akili na kupata kuamka na kukaa kuweko na kuamka ndani ya ukweli wa maisha.
Kama sehemu muhimu ya maongozi yake kuingia katika wakati wa sasa, mwandishi anachunguza ana penya kwa undani fumbo la kuwepo kwetu. Anafichua hatua zilizofichika zinazo elekeza kwa uerevu. Yeye hutoa ufahamu kwa yalio maswali mazito ambayo lazima tukumbane nayo ikiwa tutakuwa huru kabisa. Huongelea safari ya roho kwa namna iletayo maisha yote katika kutafakari na kugeuza matatizo na shida kuwa nafasi ya mwamko.
Huenda mandhari muhimu zaidi ya kitabu hiki ni utambuzi wa kipekee wa mwandishi wa hali ya akili na nafsi. Anaelezea kwa kinaganaga jinsi kusifa kwa nafsi kuwa macho ndiyo zizuizi cha msingi cha mwamko na vile tunaweza kushinda huku kusita kwa namna iliyo rahisi na ya kufaa.
Kila kurasa la kitabu hiki kinafichua sehemu ya fumbo. Kuna utaratibu unaoelekeza katika mwamko katika kila kurasa. Ni kama ramani ielekezayo nyumbani.
MAFUNZO YA LEONARD
Tunapokuwa katika ile dunia ya kutafakari akilini, tuko mahali ndani ya wakati uliopita au wakati ujao unaodhaniwa. Tuko katika dunia ya mawazo, kukumbuka, hukumu na kuamini hatuko hapa sasa. Tunachopata kuona sio ukweli na uhalisi wa wakati uliopo.
Hakika, wakati uliopita hujipenyeza ndani ya matukio ya wakati uliopo na kuupotoza. Yale yote tunayo sadiki hutufunga na uchungu tuliopata kuona katika wakati uliopita hubadili kwa ubaya tunavopata kuona maisha.
Mwamko ina maana kuwa kuamka toka dunia ya kuwaziwa akilini tu, kuingia ile ya wakati uliopo. Hii haimaanishi kuwa usikumbuke yaliyopita au usikuwe na matarajio ya wakati ujao. Ungali unashiriki katika dunia ya wakati lakini hauhusishwi wala kuainishwa na mambo yaliyokwisha pita ama matarajio ya wakati ujao. Unakuja kujitambua kama yule anayeishi katika wakati wa sasa. Unajua kwamba ni wakati uliopo pekee ambao unaweza kukutosheleza kwa hivyo unaweza kuchagua kuishi katika wakati uliopo vilivyo. Wakati uliopo unapata kuwa msingi wa maisha yako.
Unapoamka, mtazamo wa maisha yako na ulimwengu hubadilika. Uwoga, wasiwasi na mzozano hupotea unapoingia katika dunia ya mapenzi, amani na kutosheka. Unakuja kujijua kama pendo. Unakumbana na uwepo wa mungu uishie ndani yako na ndani ya kila kitu karibu na wewe. Utengamano hupotea unapoingia katika kuwa kitu kimoja. Hii ndio maana ya kuerevuka. Ni kile kilicho ongelewa na buddha. Ni kile kilicho ongelewa na Yesu. Ni kile kilicho zungumiziwa na Lao-Tzu na Krishna. Ndicho Abrahamu aliahidiwa na Mungu.
Mwamuko haihusishi mambo mengi. Uponyaki upo katika njia zisizo eleweka. Lakini kuna hatua ambazo kila mmoja wetu ni sharti kuzichukuwa.
Hatua ya kwanza na muhimu ni kujua, kupitia matukio yako mwenyewe, hali ya kuzinduka in hali ya unyamavu, amani na utulivu. Ninaweza kuonyesha hali hii kwa kupisha uwongozi, lakino sio kwa njia inayoendeleza kutegemeana au kukataliwa wa aina yotote.
Hatua ya pili ni kuwa na uhusiano mwema na hali zako kama vile nafsi yako, fikira zako, na hisia zako. Ni lazima ulete upendo na kukubalika katika kila hali yako. Kila hukumu ya nafsi yako na wengine lazima ikome ikiwa utaamka ndani ya ukweli wa maisha.
Hatua ya tatu ni kuelewa kufaao. Tu watu walio katika safari isiyo ya kawaida. Wakati unapotambua hali halisi ya safari yako, utaanza kuamka. Kila jambo ambalo limewahi kutendeka maishani mwako litaanza kueleweka. Utaanza kuona matatizo na magumu katika maisha yako kama nafasi za kukifunza na kuamka katika umoja.
Hatua ya nne ni kuwa sambamba na sheria za maisha duniani. Ikiwa utaamka vikamilifu ni lazima kuishi katika ukamilifu/uzima katika kila hali ya maisha yako.
WITO WA KUWEKO
Kuamka kikamilifu na kuelimika ina maana kuwa kuweko katika wakati wa sasa. Kuweko ni jambo rahisi sana. Ni hali yako ya asili.
Kila wakati, una chaguo. Utakuweko katika ukweli na uhalisi wa wakati huu ama utakubali nafsi yako kudanganyika katika ulimwengu wa kudhaniwa? Mafikira yote hukuondoa toka wakati wa sasa. Ukiamini haya mafikira, ambayo wengi wetu huamini, unapotea katika dunia ya kudhaniwa.
Wengi wetu tuna mazoea ya kufikiria mpaka mafikira hayaishi kamwe. Mafikira yana maisha yao. Huwa hatuchagui kufikiri kufikiria hufanyika bila ya sisi kujua toka fikra moja hadi nyingine, bila ya sisi kupata kuonja utakatifu wa wakati huu.
Wakati uliopo hauna ukumbusho wa nyakati zilizopita na mafikira ya wakati ujao. Uchungu na upungufu wa wakati uliopita hupotea ukiwepo. Wasiwasi wa wakati ujao pia hupotea. Uko hapa sasa kikamilifu katika wakati uliopo. Wakati unapokuweko kikamilifu, unapata amani, upendo, kukubalika, nguvu, ukweli na huruma. Utengamano na uwoga hupotea. Unaishi katika umoja.
Wakati unapojileta kikamilifu katika wakati uliopo, mafikira hukoma na akili yako huwa kimya, lakini kuna utulivu mkuu unaongoja kuchipuza. Akili yako inapo tulia mlango fulani wa ndani hufunguka na kupisha utulivu wa milele kuchipuza. Utulivu wa milele ndiyo asili ya kuweko kwako. Ni hali yako ya asili ndiyo asili ya kuweko kote. Ni kuweko katika utulivu wa milele wa dhamira safi. Ndiyo 'mimi ndiye' yako. Ni nafsi yako ambayo huishi katika umoja wa yote yalioko. Ni asili yako ya Buddha. Ni Kristo wa nafsi yako ambaye huishi katika umoja na mungu. Ni mwanamume au mwanamke aliye zinduka.
KUJIWEKA HURU NA MATUKIO YALIYOPITA
Ukweli ni kwamba, hatuna maisha nje ya wakati uliopo sasa. Hivi karibuni ama baadaye, sote tutakubaliana na ukweli huu.
Ikiwa utaamka kwa ukamilifu katika wakati uliopo, na kubaki katika wakati huu, lazima ujiweke huru toka matukio yaliyopita ambayo yanakutatanisha. Sio matukio yaliyopita ya kweli. Unapo fikiria, unakumbana na zama zinazokumbukwa. Utalazimika kujiweka huru na mambo unayotarajia katika wakati ujao wakudhaniwa ambayo ni matukio yaliopita kuvurumishwa mbele. Kwa ufupi ni ndoto.
Wakati ujao halisi haupatikati kwenye dunia ya kudhania. Wakati ujao halisi hujitokeza kupitia wakati uliopo, kama vile wakati uliopita waweza kujitokeza kupitia wakati uliopo.
Kuweza kukiweka huru na mambo yaliyopita kuta hatua ambazo ni lazima kupitia.
- Hisia za wakati uliopita ambazo umeweka ndani yako ni lazima uzipe nafasi kuchipuza. Haujaribu kutupilia mbali hisia hizi bali kuzipa nafasi ili zijionyeshe. Kila kitu kilicho kila haki ya kuweko, hata hisia za mahitaji, uchungu na hasira. Ikiwa hazikuchipuza ulipokuwa mchanga kwa sababu ya uchungu uliokuwa nao wakati huo au kwa sababu haukuzipa nafasi kuchipuza ni lazima zipewe nafazi kuchipuza.
- Msamaha una nguvu unaoweza kukuweka huru na mambo yaliyopita. Samehe wale wote ambao wamekukosea na uombe msamaha kutoka wote uliowakosea. Msamaha lazima uwe wa kweli. Wakati mwingine ni lazima upitie uchungu na hasira kwa wale waliokukosea kabla ya msamaha.
- Kwa watu wengine, kutulizwa wa nafsi kutokata na mambo yaliyopita huwa ni muhimu kabla ya msamaha. Habari njema ni kwamba, kupitia nguvu wa mwamko ambayo ni hali ya umoja na mungu, uponyaji wa moyo na hisia inawezekena kwa njia zisizoweza kueleweka au kuaminika. Katika kutenda kazi na watu wengine kumeshuhudia haya katika maisha yao.
- Ukibakia katika dharau, hatia au lawama huwezi kuwepo katika wakati uliopo kwa sababu hisia hizi hukufunga katika wakati uliopita lazima hizi hisia zichipuze. Zikumbuke kwa mapendo na kwa njia ya kukubali. Tambua, miliki, kiri na uonyeshe hisia hizi lakini usiziwekelee kwa yeyote. Usiziamini unazikumbuka ndiposa zisiwe zimefichwa kamwe kwahivyo haziwezi kukutawala bila ya wewe kujua. Hisia za chuki, lawama na majuto huonyesha kuwa haujachukuwa wajibu wa maisha yako. Ni rahisi kumlaumu mtu mwingine kuliko kuwajibika.
- Hatua ifuatayo ni ngumu kuweleweka na ndiyo inayokataliwa kwa urahisi. Ukiendelea kupata hisia za furaha kwa kukumbua matukio ya furaha yaliyopita, utabakia katika utumwa wa akili na majivuno milele. Kujihusisha na kumbukumbu za furaha hukuweka katika dunia ya kudhania na kufungia kumbukumbu za huzuni na uchungu ambazo haungependa kukumbana nazo. Hii ni kwa sababu akili ni dunia ya uwili na hakuna njia ya kuepuka uwili huu isipokuwa kuweko kikamilifu hadi umoja ambao ndiyo msingi wa kuishi ujionyesha. Ni sawa na kupata raha kutokana na matarajio ya matukio yajayo. Kati uliopo pekee, ndiyo unaoweza kukujaza, ni katika mwamko mkamilifu pekee ndiyo uwili hushindwa na umoja kuchipuza.
KUWEKO KIKAMILIFU INA MAANA GANI?
Kuweko ni kuamka katika sehemu ya maisha yako ambayo hushinda akili zako. Umetulia na upo, kikamilifu na kile kilicho hapa sasa. Ikiwa upo kikamilifu hakuna wakati isipokuwa wakati huu. Hii ndiyo maana yake kuwa macho katika ukweli wa maisha. Upo kikamilifu hadi unaishi katika wakati huu pekee. Una amka daima. Katika hali hii ya mzinduko matukio yaliyopita pamoja na matarajio ya wakati ujao hupotea na wakati uliopo pekee ndiyo unaoweza kupata. Huwezi hudumu katika dunia ya wakati kwani hakuna wakati. Hauna faida mbali na wakati huu. Haimaanishi kuwa aliye zinduka huwa katika hali ya kuweko kila mara. Inawezekana kuhudumu katika uwepo usiokuwa mkamilifu ndiposa dunia ya wakati bado upo katika sasa na wakati uliopo utatambulika kama ukweli wa maisha.
Ikiwa umezinduka kimsingi katika wakati uliopo unaishi bila hukumu, woga na tamaa. Unaishi katika hali ya kukubali. Unaishi kama pendo ulimwenguni. Mawazo ya utengamano yanapotea. Unaishi na hisia ya umoja wa kila kitu na kuendelwa kujua kuishi kwa milele. Unaona wengine wakiwa sawa na wewe na walio werevu hata kama hawafahamu haya. Hii hujumulisha wanyama na mazingira. Ni vigumu kumdhuru mwenzio kwa kupenda. Una huruma na unatenda kwa busara. Huwezi danganya. Kuna kitu ndani yako ambacho hakiwezi kukuruhusu kutenda haya. Unapo amka kimsingi katika ukweli wa maisha unakuwa huru na majivuno.
Hii haina maana kuwa aliyezinduka amekamilika. Wakati mwingine waweza geuka hali na uwe na uwoga na ukose uhakika ama uwe na hisia za uchungu na hasira. Lakini tofauti ni kwamba unafahamu kuwa hali hii ya utengano sio ya kweli na ni ya muda mchache tu. Hauamini ile hali uliyo nayo. Unajuwa wakati uliopita unajitokeza kwa namna fulani katika wakati uliopo. Haujihusishi na matukio hayo ama hisia zitokanazo na matukio hayo. Na ungali unawajibika na mambo yote unayopitia. Haya matukio yanaaminika na kukubalika lakini sio kukubalika kama ndiyo ukweli. Katika mabadiliko ya mara kwa mara unajijua kama asiyebadilika.
UPONYAJI WA MOYO
Unapozidi katika mzinduko, mambo yaliyopita ambayo hayakusuluhishwa hujitokeza kwa sababu za uponyaji na ukamilisho. Hii hujumlisha uponyaji wa majeraha ya hisia toka uhusiano wako na wazazi wako ama mambo mengine ya kuhuzunisha utotoni mwako.
Ijapokuwa, chanzo cha mzozo wakati mwingine huwa ni maisha ya zamani.
Katika warsha za kibinafsi, majeraha na mambo ambayo hayakusuluhishwa toka maisha ya zamani yanaweza kujitokeza kwa uponyaji na ukamilisho. Kwa njia iliyo rahisi na kwa upole, Leonard anakuongoza katika uponyaji wa maisha ya zamani. Moyo unapona, na pia unapona na kuwa huru maishani mwako. Ukipokea uponyaji kupitia njia hii unakuwa huru tokana na matukio ya zamani. Basi kuweza kuweko katika wakati uliopo. Inaelekeza katika amani na kuwekwa huru, kitu ambacho ni cha maana sana.
Hatimaye, utakuja kujua kuwa matatizo na magumu yaliyotokea maishani mwako ni fursa ya uponyaji na kupata mafunzo ya moyo ambayo unaishi kujifunza katika haya maisha.
Kwa kweli wewe ndiyo mshindi wa moyo wako. Kuzinduka kikamilifu katika haya maisha ni kunusuru moyo wako katika kudumu kwake milele.
MPISHO WA HALI YA MZINDUKO
Ukihudhuria warsha za Leonard unaingia katika hali ya mzinduko
Kinachotendeka ni kwamba nguvu zitokanazo na kuweko kwa Leonard zinaita sehemu yako iliyokamilika. Imekuweko ndani yako tangu zamani, lakini umehusika na dunia ya kudhaniwa na kujitenga na kupitia hali hii. Umejizuia kujiboresha zaidi.
Ukisha shuhudia hali ya kuzinduka hata kama ni kwa lisali tu au masaa mawili wakati wa warsha, ama mahojiano ya binafsi au mazungumzo ya simu, itajenga msingi wa mzinduko wako.
Kuna hatua mbili zinazoelekeza katika mwamko
Hatua ya kwanza ni kufahamu kutokana na matukio yako hali ya mzinduko. Katika hali hii upo kikamilifu na kutulia katika umoja. Utengano unapotea. Umezinduka katika kuwepo kwa MIMI NDIYE. Umezinduka katika ufahamu wa kristu. Kupitia hali ya mzinduko ni muhimu katika safari ya mwamko.
Hatua ya pili ni kutambua ni wakati gani na ni vipi unapoteza ushirikiana na hali hii ya mwamko. Ni mambo gani, fikira, hisia, matamanio au uwoga unaokufunga katika dunia ya kudhania? Ni nini ambacho hukutoa toka wakati huu kwenda zama zilizopita au matarajio ya wakati ujao?
Hizi hatua mbili hutegemeana, Leonard huziita hatua mbili za randa ya mwamko.
WARSHA
Kushiriki kongamano pamoja na Leonard hutoa nafasi ya kujitumbukiza katika kuwepo na uponyaji na kuwa huru na mambo yaliyopita. Mafunzo ya Leonard ni ya kipekee, rahisi na ya moja kwa moja. Mara mbili au tatu kwa mwaka, utakuwa na fursa ya kushiriki warsha ya siku tatu au tano. Warsha hizi ni za wale ambao wamejipa sharti katika mwamko wao. Zina changa moto, furaha, zinaponya na ni nafasi ya kubadilisha maisha kuliko chochote kile umewahi kudhania. Katika warsha hizi unaweza husika kwa kubaki kimya, unaweza kuuliza maswali ama unaweza jadili chochote kinachohitaji uponyaji na kuwekwa huru. Cha msingi ni kuwepo kwako, na kujitumbukiza katika kuwepo. Mtu amewahi kusema kuwa; kuwa pamoja na Leonard ni kama kuogelea ndani ya uwepo. Lakini kazi ya Leonard sio tu kuhusu kuwepo.
Kipande kifuatacho kilichoandikwa na Leonard, kinaonyesha kazi hii inahusika na nini na kinachohusishwa katika mwamko wa kweli.
Hatua mbili za randa ya mwamko
"Mimi hufunza hatua mbili za randa ya mwamko. Hatua ya kwanza ni kuchagua wakati uliopo kama ukweli wa maisha. Kuzidi na kuzidi kila siku, unachagua kuwepo katika wakati uliopo, badala ya kupotea katika mawazo. Hii ina maana kuwa itakubidi kuamuwa kupepo wakati mwingi kila siku, hadi uwe na uzowefu ambao hautategemea uamuzi wako. Hali yako ya kiasili ni kuwapo. Kuwepo na kuzinduka kikamilifu ni rahisi ni ya mara moja. Halihitaji mazoezi. Ni kukumbuka wenye utulivu.
Lakini kubaki katika hali ya kuwepo katika maisha yako ya kila siku na katika ukoo wako sio rahisi sana. Watu wengi hubaki katika hali ya kuwapo kwa muda mfupi huwa sio muda mrefu kabla ya kuvutwa bila mapenzi yako toka kuwapo hadi hali ya tafakari za akilini. Kwa mara nyingine una kadiriwa na hisia za huzuni zilizopita na imani pungufu. Kwa mara nyingi unapotea katika zama zako na matarajio ya wakati ujao. Kwa mara nyingine unafungwa katika ukoo wako. Kwa mara nyingine unanaswa katika mazingaombwe hiyo ndiyo sababu ya umuhimu wa hatua ya pili ya randa ya mwamko. Hatua ya pili naiita "kutenda kazi"
Hatua ya pili huhusisha kuleta katika tafakari njia zote ambazo wewe huvutwa toka kuwapo. Ni upambo upi ambao hukuvuta kurudi dunia ya kudhaniwa akilini? Nini hukuzuia kuwa na kuwapo madhubuti ya daima? Hadi haya maswali yajibiwe, vipi unaweza kuzinduka iwapo sio kwa mda mfu kila mara?
"Hatua ya kwanza huelekeza katika kuwapo. Hatua ya pili huelekeza katika ustadi."